Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Hujjatul-Islam wal-Muslimin Arif Hussein Wahidi, Makamu wa Rais wa Baraza la Maulamaa wa Kishia wa Pakistan, katika mkutano wa kitaifa wa umoja uliofanyika katika mji wa Rawalpindi Pakistan, alitaja umoja wa Umma wa Kiislamu kuwa ndio njia pekee ya kukabiliana na maadui, na akatoa wito wa kutekelezwa kwa vitendo ujumbe wa Qur’ani na waislamu.
Alianza hotuba yake kwa kusisitiza juu ya mafundisho ya Qur’ani, akaashiria nafasi adhimu waliyonayo waislamu na kusema: "Qur’ani Tukufu imetutaja kwa majina mazuri kama vile "Umma moja", "Umma bora", na "Umma wa kati"." Hata hivyo, tunapaswa kujiuliza: Je, kwa vitendo, sisi leo ni Umma mmoja, au tumegawanyika katika madhehebu, makundi na itikadi za kimadhehebu?
Mwanachuoni huyu kutoka Pakistan alisisitiza kuwa umoja wa Umma wa Kiislamu si kauli tu ya maneno, bali ni kanuni ya vitendo ambayo inapaswa kutekelezwa katika maisha ya kisiasa, kijamii na kidini kwa waislamu.
Aliendelea kwa kusema: "Iwapo umoja wa kweli utadumishwa kati ya Waislamu, basi maadui wa Uislamu, hasa Marekani na Israel, wataelewa kwamba Waislamu ni watoto wa dhehebu moja la Kiislamu, na njama zao haziwezi kuuvunja umoja huu.
Maoni yako